NEEMA YA ASUBUHI Linus Siwiti's podcast

13/06/2021 15 min
NEEMA YA ASUBUHI Linus Siwiti's podcast

Listen "NEEMA YA ASUBUHI Linus Siwiti's podcast"

Episode Synopsis

10 Hatimaye, mzidi kuwa hodari katika Bwana na katika uweza wa nguvu zake. Waefeso 6:1011 Vaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kuzipinga hila za Shetani. Waefeso 6:1112 Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho. Waefeso 6:1213 Kwa sababu hiyo twaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kushindana siku ya uovu, na mkiisha kuyatimiza yote, kusimama. Waefeso 6:1314 Basi simameni, hali mmejifunga kweli viunoni, na kuvaa dirii ya haki kifuani, Waefeso 6:1415 na kufungiwa miguu utayari tupatao kwa Injili ya amani; Waefeso 6:1516 zaidi ya yote mkiitwaa ngao ya imani, ambayo kwa hiyo mtaweza kuizima mishale yote yenye moto ya yule mwovu. Waefeso 6:1617 Tena ipokeeni chapeo ya wokovu, na upanga wa Roho ambao ni neno la Mungu; Waefeso 6:1718 kwa sala zote na maombi mkisali kila wakati katika Roho, mkikesha kwa jambo hilo na kudumu katika kuwaombea watakatifu wote; Waefeso 6:18