Kumshinda Mshtaki.

02/12/2023 10 min

Listen "Kumshinda Mshtaki."

Episode Synopsis

Katika Mwanzo sura ya 38, Tamari, ambaye alikuwa mjane mara mbili, anashtakiwakuwa kahaba. Mume wake wa kwanza Eri aliuawa na Yahweh kwa sababu alikuwa mwovu. Ndugu yake mdogo Onan ambaye alipewa Tamari aliuawa na Yahweh kwa sababu alishindwa kutekeleza wajibu wake wa kumlea mtoto wa kiume kwa heshima ya marehemu kaka yake na mke wake Tamari. Sasa Tamari ambaye alikuwa hana mume kwa muda mrefu agundulika kuwa ana mimba. Anashtakiwa mbele ya baba-mkwe wake Yuda, ambaye anatangaza na anatazamia kutumia adhabu ya kifo. Katika hali ya kushangaza ya hadithi hii kuhusu mjane mjamzito, Tamari anawashinda washtaki wake kwa kuonyesha kwambaYuda, yeye baba mkwe, alikuwa kuwajibika kwa ujauzito wake.