Episode 17 - Tafakari ya Maandiko Ya BibliaLinus Siwiti's podcast

30/07/2020 14 min
Episode 17 - Tafakari ya Maandiko Ya BibliaLinus Siwiti's podcast

Listen "Episode 17 - Tafakari ya Maandiko Ya BibliaLinus Siwiti's podcast"

Episode Synopsis

18 Kuna mambo matatu yaliyo ya ajabu kwangu, Naam, kuna manne nisiyoyafahamu. Mithali 30:1819 Mwendo wa tai katika hewa; Na mwendo wa nyoka juu ya mwamba; Mwendo wa merikebu katikati ya bahari; Na mwendo wa mtu pamoja na msichana. Mithali 30:1920 Hivyo ndivyo mwendo wa mwanamke mzinifu; Hula, akapangusa kinywa chake, Akasema, Sikufanya uovu. Mithali 30:2021 Kwa ajili ya mambo matatu nchi hutetemeka, Naam, kwa ajili ya manne haiwezi kuvumilia. Mithali 30:2122 Mtumwa apatapo kuwa mfalme; Mpumbavu ashibapo chakula; Mithali 30:2223 Mwanamke mwenye kuchukiza aolewapo; Na mjakazi aliye mrithi wa bibi yake. Mithali 30:2324 Kuna viumbe vinne duniani vilivyo vidogo; Lakini vina akili nyingi sana. Mithali 30:2425 Chungu ni watu wasio na nguvu; Lakini hujiwekea chakula wakati wa hari. Mithali 30:2526 Wibari ni watu dhaifu; Lakini hujifanyia nyumba katika miamba. Mithali 30:2627 Nzige hawana mfalme; Lakini huenda wote pamoja vikosi vikosi. Mithali 30:2728 Mjusi hushika kwa mikono yake; Lakini yumo majumbani mwa wafalme. Mithali 30:2829 Kuna watatu wenye mwendo wa kupendeza, Naam, wanne walio na mwendo mzuri. Mithali 30:2930 Simba aliye hodari kupita wanyama wote; Wala hajiepushi na aliye yote; Mithali 30:3031 Jimbi aendaye tambo; na beberu; Na mfalme ambaye haasiki. Mithali 30:3132 Ikiwa umefanya kipumbavu kwa kujikuza; Au ikiwa umewaza mabaya; Basi weka mkono wako juu ya kinywa chako. Mithali 30:32